Mkataba mpya REA na Silopower Limited.

Mkataba mpya REA na Silopower.

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (Rea), Hassan Saidy akimkabidhi mkataba Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Silo Power Ltd, Mmbalo Msuya (kulia), wakati wa hafla ya utiaji saini kwa makandarasi kwa ajili ya kuwaongezea muda ili kukamilisha mradi wa Rea wa tatu wenye thamani ya Sh 1.5 trilioni ulioanza kutekelezwa Julai 2021. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) Janet Mbene.

Wakandarasi Wakandarasi wanaotekeleza Miradi ya Kupeleka Nishati ya Umeme Vijijini kwenye mikoa ya Mikoa ya Mtwara, Tanga, Morogoro, Kigoma, Tabora wametakiwa kukamilisha miradi hiyo ili wananchi waweze kupata huduma ya umeme ndani ya kipindi cha Miezi Mitatu.

Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Janet Mbene ameyasema hayo Leo Jijini Dar es Salaam kwenye kikao cha kujadili changamoto za utekelezaji wa miradi ya kusambaza umeme Vijijini pamoja na utiaji Saini nyongeza za kazi katika mikataba.

“Tupo hapa chini ya Wizara ya Nishati kusimamia miradi ya REA je na sisi tunafanya kazi yetu? tumetoka kupitisha bajeti ya Wizara yetu ya Nishati. Na kabla ya hapo tulikuwa na maonesho ya wiki ya nishati pale kwenye viwanja vya bunge.
Wabunge wengi waliingia pale walitazama walikuwa wakiuliza maswali wakaleta hoja zao mbalimbali tuliwajibu kwa kiasi kikubwa wengine walifurahi sana. Na wengine kwa sababu ninyi ndugu zangu (wakandarasi) hamjafanya kazi yenu kikamilifu.

“Kama kila mmoja angefanya kazi yake vizuri tusingepaswa kusemana. Imebidi tufanye kazi ya Ziada ya kukutana na wabunge husika tukawaita na wakandarasi husika ili kukubaliana kwamba tunafanyeje?

“Tumekubaliana kufanya kazi miezi Mitatu. Wale ambao mmekuwa mkisuasua mjitahidi mfikishe japo 60% ya kazi ambazo mmpewa kwa kipindi cha mwisho wa mwezi wa Tisa” Janeth Mbene, Mwenyekiti Wa Bodi Ya Nishati Vijijini (REB)


Leave A Comment

X